latest articles



Mwanamitindo wa kimataifa wa kiume kutoka nchini Burundi, Hakim NKENGURUTSE anaeishi nchini Afrika ya kusini (Republic of South Africa) Mkoa wa Gauteng, mji wa Johannesburg.

Zimeonekana Takriban Picha zake 6 ambazo zimezuwa gumzo mitandaoni na kudaiwa kwamba amekeuka maadili ya kitamaduni za Burundi.
Pichani, Hakim ameonekana kuvalia nguo aina ya chupi huku yupo kifua wazi na miguuni kavaa viatu vya shingo ndefu, ambapo wengi wa watu hufananisha viatu hivyo na vya kike.



\

Tumepokea maoni ya watu wengi kuhusiana na mwanamitindo huyu wa kimataifa.
Tukumbuke, ni mwakajana mwishoni ambapo mwanamitindo huyo alikuwepo hapa nchizni ziyarani baada ya kuweza kushiriki kwenye michuano ya SWAHILI FASHION WEEK awamu ya 2017.



Read more




Msanii wa Burundi anaeishi nchini Australia, South Australia, Adelaide Jelly Beatz, anatamba kwa wimbo wake Need someone's space, usiku wa kuamkia leo ameweza kubandika picha tatu za msichana mrembo aitwae Salima Issa ambae hudaiwa kuwa huwenda ndie mpenzi wake,

Baada ya kupata taarifa hizo kwenye mitandao, Baadhi ya watu walijaribu kutuuliza kuwa habari hizi ni kweli au laa?
Ambapo mpaka sasa hatujapata majibu yoyote kutoka kwa mkali huyo.
Kuna tetesi zinazosemwa kwamba mkali huyo Jelly Beatz na msichana huyo Shemeji yetu Salima wataonekana kwenye video mpya ya Jelly Beatz ambayo haijatajwa jina.

Picha kadhaa za Salima kwenye ubora wake



 








Read more




Msanii wa muziki wa kizazi kipya Gaga Blue anaetamba kwa wimbo wake IVO IVO alioshirikiana na msanii kutoka Tanzania Young D, amewataka wasanii wa muziki wa Indundi Music  kuwekeza pesa za nyingi kwenye muziki wao ili kuongeza thamani ya muziki wa Burundi.

Muimbaji huyo ameiambia ( Rundiwood) kuwa uwekezaji kwenye muziki ndiyo siri ya kufanikiwa kwa wasanii wengi na ilo tayari ameligundua kwa wasanii wengi nchini Tanzania.


Aidha msanii huyo alitoa mfano kwake na kusema kuwa mara nyingi anawekeza sana bila kujali kusaidiwa na meneja wake na akaongeza kwamba akipata milioni 6 anawekeza milioni 4 kwenye muziki huku akichukua milioni mbili kama faida ya kazi yake.





Licha ya kuzidi kutamba na kuonekana msanii wa kuigwa nchini Burundi, Gaga Blue alitoa donge kwa msanii mmoja wa Burundi bila kumtaja jina na kusema kuwa "Kuna msanii mkongwe Burundi ila hana mpango wowote kwenye muziki wakati pesa za show anazidi kuzipata ila ukitizama muziki wake hauna thamani yoyote."

Baadhi ya wafuatiliaji wa karibu wa muziki wa Indundi Music wanadai kauli hiyo ya Gaga Blue imemlenga msanii mwenzie Mugani Desire Big Fizzo jambo ambalo wengi wao kuhisi labda kutatokea utofauti wa ki kazi kati ya wawili hao.




Read more


Mwanamuziki, mtetezi wa Hip Hop Hakizimana Hubert, KING HUBERT Anaetamba kwa wimbo wake IWACU NIHEZA alio mshirikisha Jean Pierre Nimbona KIDUM KIBIDOO, baada ya ku kaa kimya kwa muda kiasi, sasa ameahidi kuanza mwaka 2018 kwa ujio mpya kabisa.



Ame ahidi kuachia wimbo mpya alio uvika jina la BELIEVE IT ambapo ameshirikiana na msanii mwenzie wa hapa hapa Burundi ila wanaishi nae huko nchini Australia ambae ni JAY TWIST.


Wimbo huo utakuja ni Audio na Video, ambapo mpaka dakika hii haijajulikana video hio imesimamiwa na muongozaji yupi.




Read more





Magic Soldier ametuletea hii hapa kutoka Mood Nation.









Read more



Tareh 30 mwezi desemba mwaka 2017, ndio siku ambayo zimetolewa tuzo za SOFT AWARD wilayani NTAHANGWA tarafa la Kamenge, maneo ya Centre Jeune Kamenge.

Hafla hio imewakusanya wasanii kem kem kwenye tasnia tofauti za sanaa.
Walikuepo waimbaji, wachora kwa wino wa ufyonzi, waigizaji Nk...


Wameanza kwa kugawa vyeti vya heshima kwa wasanii waliofanya kazi kwa kujitolea kwa moyo, ambapo Tambwe Remy amepewa cheti kama mchekeshaji bora aliefanya kazi kwa bidii

Aliefuatia ni Promotor aliejitolea kwa ku promote muziki ambapo alie nyakua cheti hiko ni Rick Love 
 

 Wengine waliopata cheti hiko ni Pierre Nkurikiye, Ami Pro, B-Face, Akes Don...
         

 


Treibeka Hill Top 10 imechukua tuzo kama management bora ya mwaka 2017, Akeza Mutima wamechukua tuzo kama Taasisi lililo jitolea kudhamini katika matamasha ya muziki wa Burundi, nafasi ya pili ni Fungus Tea.
Ilipo fika zamu ya kugawa tuzo za heshima, makundi ma nne yalio tajwa ni

* Kundi bora la kiutamaduni
* Filamu bora ilio tangaza nchi
* Kundi bora la Gospel
* Mwana hip hop bora wa mwaka.


Read more


Picha na Isaac Classic



Baada ya ku saini mkataba na management yake mpya ya TMG (Treibeka Music Group) mwaka huu mwanzoni, B-face ameonekana kushamiri kwenye muziki wa Hip Hop tangu baada ya ku achia wimbo wake ulio beba jina la LA DIFFERENCEuliompa umaarufu mkubwa nchini Burundi na Rwanda.

GIRIKWISHAKA Boniface, B-Face hajaregeza mkanda wa hip hop wala kuliachia gurudumu hilo, Alifuatisha na wimbo SIPENDI UJINGA ambao umezidi kumjenga vilivyo na akamalizia na INGOMA ZIWACU ambapo ameonekana kuwa hajabahatisha.
Kwenye kipindi cha Ahabona moment kwenye Radio Colombe, amechaguliwa na wapenzi wa muziki wa nyumbani kuwa kama mwana hip hop bora wa mwaka na kupewa tuzo ya heshima. hapo juzi tareh 29 Desemba 2017 jijini Bujumbura tarafani Mukaza, kata ya Jabe, amepewa tuzo na ku vishwa taji la heshima kama mwana hip hop bora wa mwaka, Jana pia tareh 30 Desemba kapewa Tuzo na cheti cha heshima kama msanii bora wa hip hop mwaka 2017.

Picha na Isaac Classic

Kitu hiki kimethibitishwa na watu wengi kuwa mwanamuziki huyu amefaa kunyakua tuzo hizi.


Ingoma ziwacu by B face

Read more








Mabibi na mabwana Madiba The Classic ametusogezea hii hapa mpya yake.



Read more





Imeonekana leo mchana kwenye mitandao ya kijamii Clip video yenye sekunde 53 ya Natacha La Number akim'cover A flow kwenye wimbo wake La Number, Ni baada ya picha kem kem kusambaa kwenye mitandao ya kijamii, wawili hao wakiwa sehemu za bustani A Flow akimcharazia kinanda aina ya Piano mwanadada Natacha siku ya jana.


Video inapatikana hapa chini


Tukumbuke kwamba mwanadada huyo ameahidi kumsaidia msanii huyo chipukizi A Flow kwa namna moja au nyingine, Na safari ya msaada ndio kama imeanza.

Swali ni kwamba "Natacha amegundua kitu gani kwa msanii huyo chipukizi?" wanajiuliza mashabiki wa muziki.






              
Read more



MANIRAMBONA IBRAHIM maarufu kama ICUBURUNDI, muigizaji anaetikisa tasnia ya filamu nchini Burundi, anaonekana kushamiri kwenye tasnia hii tangu baada ya filamu alioigiza na muigizaji wa kike kutoka nchini Tanzania, SHAMSA FORD, na kujipatia umaarufu mkubwa nchini nakujitangaza ki kazi nchini Tanzania ambako anaonekana mara nyingi kujielekeza huko kufanya kazi nyingine kem kem.

Tukumbuke ni mwaka jana ambapo waliweza kumleta muigizaji mwingine kutoka nchini Tanzania Hemedy Suleiman nakufanya nae Movie ambayo imepewa jina la BURUNDIAN IN DAR ila mpaka dakika hii haijajulikana ni lini itaachiwa.


Icuburundi kwasasa aliweza kuachia filamu mpya ambayo inatamba nchini GENDER EQUALITY, kama ulikua bado hujabahatika kuitazama hii hapa chini nimeikusogezea.



Read more



Baada ya kusikika FLOW SLIM kwenye wimbo wake LA NUMBER ambao inasikika kwamba alikua akimuagizia ujumbe msanii mwenzie NATACHA ambae inafahamika kwamba yupo tayari ndoani.


Leo hii al-khamisi 28 Disemba, 2017 majira ya saa tano asubuhi, zimeonekana picha kadhaa za wawili hao wakiwa sehemu kwenye bustani A flow akimcharazia kinanda Natacha kwa ishara ya kumuimbia wimbo.




Tukumbuke kwamba Natacha aliahidi kumuonyesha ushirikiano mkubwa msanii huyo ambapo hakuweza kufunguka ni aina gani ya ushirikiano...
Baada ya hapo alionekana A flow kwenye exclusive interview ya NGM TV SHOW alipoulizwa kuhusiana na wimbo huo amejibu kua ni hisia zake zaukweli dhidi ya Natacha kwa maana kwamba anampenda kwa dhati.



Kama umepitwa na interview hiyo hii hapa nimekusogezea



Read more







BUTOYI Bertin Maarufu kama Berry Prince ni mmoja kati ya wasanii wa Burundi wanaoishi na kuendeleza kazi zao za muziki huko nchini Australia, Ni kijana mashughuli anaejituma kufanya kazi nzuri ili kesho ajitangaze kimataifa.


Leo hii ametusogezea video yake mpya ya wimbo alioshirikiana na msanii mwenzie wa kike ambae ni Veronica, Hivo basi Burudika na video hii hapa chini





                 
Read more

                             


Msanii wa kizazi kipya nchini Burundi anaetamba kwa wimbo wa QU'EST CEQU'IL YA ( KESKILYA) aliomshirikisha Fizzo, Ndayisaba Junior a.k.a Mr. Champagne, Amedhihirisha wazi siku ya ijumaa pili tareh 24 disemba 2017 baada ya tamasha lililowakusanya wasanii kutoka Burundi Natacha na Vichou pamoja na msanii kutoka Jemhuri ya kidemokrasiya ya Congo Fally Ipupa, Licha ya msanii huyo Mr Champagne kuonekana kwenye picha nyingi akiwa na Fally Ipupa mitandaoni.





"Mimi ni shabiki wako mkubwa hapa Burundi" alitamka Mr Champagne akimuelezea role modele wake, kwa ku thibiti hilo Fally alimuimbia wimbo wake mmoja huku Mr Champagne aki mkatia mauno.

Hii hapa ni post alioweza kuipost siku ya jana kwenye ukurasa wake wa facebook.




  
               
Read more







Baada ya KINGORONGORO kutangaza kuwa hivi punde ataachia wimbo mpya kwa jina la VUNJA GOTI, Rapper huyo kwa muujibu wake andai sio wimbo wa kawaida, huku marappers wengine matumbo joto...


Habari tulizo nazo hapa ni kwamba kwenye wimbo huo ameshirikiana na Producer pia Msanii ambae ni KOLLY THE MAGIC, na wimbo huo utaachiwa AUDIO & VIDEO, ila bado hajatangaza ni lini atauruhusu.

Mashabiki wa muziki wa nyumbani wameanza kutumia jina la wimbo huo kama SLOGAN kwenye mitandao ya kijamii hata mitaani kwao pia ku dhihirisha ni jinsi gani wanavyo usubiri kwa hamu.

Tukumbuke kwamba ni hapo juzi tu ambapo msanii huyo alipoweza kuachia wimbo wake mpya kwa jina la KALI NA NUSU ambao haujachukua hata wiki mbili mara ghafla ametangaza atauachia wimbo mwingine.



                  
Read more